Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa (ICPAC) kulicho chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) jana kimesema, nchi kadhaa za Pembe ya Afrika zinatazamiwa kukumbwa na wimbi la joto kali kutokana na kuongezeka kwa hali ya joto.
Katika utabiri wake wa karibuni, ICPAC ilitabiri kuwa wimbi la joto kali litatokea katika siku zijazo licha ya ukweli kwamba nchi nyingi za eneo hilo zinakabiliwa na mvua kubwa kuliko kawaida wakati wa msimu wa mvua kutoka mwezi Machi hadi mwezi Mei.
ICPAC imetabiri kuwa halijoto inatarajiwa kuongezeka katika maeneo ya kusini mwa Somalia, kusini-mashariki mwa Kenya, eneo la Afar nchini Ethiopia na maeneo ya kaskazini mwa Sudan Kusini. ICPAC pia imeongezeka kuwa halijoto ya wastani inatarajiwa kufikia nyuzi joto 32.