Msomi wa Somalia: “Nguvu mpya ya Uzalishaji” itaihimiza China kupata maendeleo mapya na kunufaisha nchi nyingine duniani
2024-04-10 09:53:00| CRI

Wazo la “Nguvu mpya ya Uzalishaji” lilitolewa kwa mara ya kwanza na rais Xi Jinping wa China wakati alipofanya ukaguzi mkoani Heilongjiang mwaka 2023, na limewekwa katika ripoti ya kazi ya serikali ya China katika mwaka huu, na kuorodheshwa kuwa kazi kuu ya kwanza kati ya kazi kumi kwa jumla.

Msomi wa Somalia Abdilahi Ismail Abdilahi alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Shirika Kuu la Utangazaji la China(CMG)amesema, maendeleo ya haraka yaliyopatikana nchini China katika miaka miongo kadhaa iliyopita yamefuatiliwa na watu duniani. Sasa rais Xi ametoa wazo la “Nguvu mpya ya  Uzalishaji”, ambalo litaleta ushawishi mkubwa kwa mchakato wa kisasa nchini China. Wazo hili litahakikisha China inaweza kusonga mbele, na pia limetoa mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea duniani zikiwemo nchi za Afrika. Anaona kama nchi za Afrika zitafuata njia ya kujiendeleza ya China, zinaweza kuendana na mwenendo wa maendeleo ya dunia na kujitokeza duniani.

Pia anaona wazo la “Nguvu mpya ya Uzalishaji” si kama tu litaihimiza China kufungua safari mpya ya maendeleo, vilevile litachangia maendeleo ya nchi nyingine duniani.