Jeshi la Magereza nchini Uganda (UPS) limesema zaidi ya wafungwa 5,000 nchini humo wamegundulika kuwa na ugonjwa wa macho mekundu.
Msemaji wa Jeshi hilo Frank Baine amesema, kesi hizo zimethibitishwa katika magereza mbalimbali nchini humo. Amesema kati ya kesi 5,905 zilizothibitishwa, wafungwa 4,704 wamepona, na wengine 1,201 wako katika hali mbaya.
Baine amesema, Jeshi la Magereza linafuata kikamilifu vigezo vya utendaji na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya ili kudhibiti mlipuko huo.
Ameongeza kuwa, ingawa bado watu wanaruhusiwa kutembelea wafungwa, lakini amewashauri kukaa mbali na magereza kama tayari wamepata maambukizi ya ugonjwa huo.