Jeshi la Israel lasema litaendeleza operesheni zake katikati mwa Gaza
2024-04-11 10:47:21| cri

Vikosi vya Israel vimesema vitaendelea na operesheni za kijeshi katika eneo la kati la Ukanda wa Gaza, huku kundi la Hamas likisema limeanzisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Israel kaskazini mwa Ukanda huo.

Jeshi la Israel limesema limeharibu maeneo ya kundi la Hamas na kuwaua wapiganaji wengi wa kundi hilo. Aidha, katika siku za karibuni, jeshi hilo limeendelea kufanya operesheni za kijeshi za angani na ardhini huko Necharim katika Ukanda wa Gaza.

Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Vita la Israel Bw. Gantz, amesema operesheni za jeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza zitaendelea kwa muda mrefu hadi kundi la Hamas litakapotokomezwa.