Kundi la 45 la Jeshi la Majini la China limewasili katika bandari ya Tuamasina, Madagascar jana na kuanza ziara ya kirafiki ya siku tano.
Katika hafla ya kuwakaribisha, Madagascar iliandaa ngoma ya Dragon na Simba, na dansi ya mtindo wa kienyeji, na wawakilishi wa wanafunzi waliwavisha mataji ya maua makamanda wa jeshi hilo.
Wakati wa ziara hiyo, pande hizo mbili zitafanya shughuli mbalimbali zikiwa ni pamoja na kutembelea kambi za jeshi na kufanya mashindano ya kirafiki ya michezo, pia wanajeshi wa majini wa China watatembelea shule za wanafunzi wenye asili ya kichina.