Mali yasitisha shughuli za vyama vya siasa mpaka itakapotangazwa baadaye
2024-04-11 10:46:05| cri

Msemaji wa Serikali ya Mali Abdoulaye Maiga ametoa taarifa akisema, serikali ya kijeshi ya nchi hiyo imesimamisha shughuli zote za vyama vya siasa.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana jioni imesema, shughuli hizo zimesitishwa mpaka itakapotangazwa tena baadaye, na shughuli zote zenye asili ya siasa pia zimesitishwa kwa lengo la kudumisha utaratibu wa kijamii.