Ufilipino yatakiwa kuacha vitendo vya uchochezi katika suala la Bahari ya Kusini
2024-04-11 14:40:20| cri

Hivi karibuni, Marekani, Japani, Australia na Ufilipino zilifanya zoezi la kwanza la pamoja la kijeshi katika Bahari ya Kusini. Vyombo vya habari vya Ufilipino viliripoti kuwa, nchi nne kuonesha kwa pamoja nguvu ya kijeshi kunalenga kuizuia China. Pamoja na mkutano wa kilele wa Marekani, Japani na Ufilipino utakaofanyika huko Washington, jaribio la Ufilipino la kutumia nguvu ya nje kuingilia suala la Bahari ya Kusini na kufanya mvutano wa Bahari hiyo kuwa la kimataifa limewekwa wazi.

Tangu mwaka jana, Ufilipino imeendelea kufanya uchokozi katika eneo hilo la bahari, ikivamia eneo lililoko karibu na kisiwa cha Huangyan na miamba ya Ren’ai. Je, lengo la Ufilipino kufanya uchokozi katika sehemu nyingi za Bahari ya Kusini ni nini? Wachambuzi wanasema, Ufilipino inataka kuleta matatizo kwa China kupitia mfululizo wa uchokozi, na kuendelea kufanya suala la Bahari ya Kusini lipambe moto.

Ufilipino inasema kutafuta amani ya kikanda kwa maneno, lakini hatua yake halisi ni kuleta mvutano. Chanzo kikuu kilicho nyuma yake ni nguvu za nje ikiwemo Marekani, ambayo inaichochea na kuunga mkono nchi hiyo. Wachambuzi wanasema, Ufilipino inategemea kwa kiasi kikubwa nchi kubwa za nje katika nyanja za jeshi na usalama, nchi hizo za nje zinadhibiti Ufilipino kupitia utoaji wa msaada, zoezi la pamoja la kijeshi na safari za pamoja baharini. Sera za Ufilipino kuhusu Bahari ya Kusini zimekuwa chombo cha umwamba cha Marekani kuikandamiza China.

Kwa upande mmoja, nchi nyingi za jumuiya ya ASEAN zinafanya juhudi kulinda amani na utulivu wa kikanda, kuhimiza ushirikiano wa kikanda na mafungamano ya kiuchumi. Kwa upande mwingine, kutokana na uchocheaji na uungaji mkono wa nchi kubwa za nje, Ufilipino imetumiwa kama nyenzo ya kuvuruga hali ya Bahari ya Kusini, ikienda kinyume na mahitaji ya kanda zima.