Maonyesho ya 135 ya Uingizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China kufunguliwa tarehe 15 mwezi huu mjini Guangzhou
2024-04-11 10:46:47| cri

Maonyesho ya 135 ya Uingizaji na Uuzaji nje wa Bidhaa ya China (CIEF) yatafanyika mjini Guangzhou kuanzia tarehe 15 mwezi huu hadi tarehe 5 mwezi ujao.

Maonyesho ya awamu hii yameshirikisha kampuni zaidi ya elfu 29 kutoka nchi na kanda 50. Kati yao, kampuni takriban 3,600 zinashughulikia mambo ya teknolojia ya kidijitali na utengenezaji wa akili bandia, na bidhaa zaidi ya elfu 90 za akili bandia zitaonyeshwa kwenye maoneysho hayo. Bidhaa hizo ni pamoja na mkono bandia unaotumia teknolojia ya akili bandia, vifaa vya usafiri vyenye mfumo wa kujiendesha wa urambazaji na vifaa vya kutafsiri lugha vya akili bandia.

Pia katika maonyesho hayo, bidhaa mpya zaidi ya milioni moja zinatarajiwa kuonyeshwa kwa watu watakaotembelea maonyesho hayo.