Askari wa kulinda Amani wa China nchini DRC wapewa Tuzo ya Amani ya Umoja wa Mataifa
2024-04-11 23:45:00| cri

Kikosi cha 27 cha askari wa kulinda Amani wa China katika Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kimepewa Tuzo ya Amani ya Umoja wa Mataifa jumanne wiki hii.

Hafla ya kutoa tuzo hiyo ilifanyika katika kambi ya uhandisi ya kikosi cha China iliyoko pembezoni mwa Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na kiongozi wa MONUSCO, Bintou Keita amesema, katika miaka 21 iliyopita, askari wa kulinda Amani kutoka China wamekuwa mfano wa kujitolea na utaaluma kupitia majukumu yao.

Ameishukuru serikali ya China kwa kupeleka askari wa kulinda Amani katika mkoa wa Kivu Kusini tangu mwaka 2003.