EAC yafikiria kuifanya siku ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Ruwanda kuwa Siku ya EAC
2024-04-11 08:37:11| cri



Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana imetoa taarifa ikisema, inafikiria uwezekano wa kuifanya tarehe 7 Aprili ya kila mwaka kuwa Siku ya EAC katika maadhimisho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.

Katika taarifa iliyotolewa jumanne na Jumuiya hiyo, naibu katibu mkuu wa EAC Bw. Andrea Aguer Ariik Malueth alitoa ahadi hiyo jumapili wakati wa kuadhimisha mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Bw. Malueth amesema, ombi rasmi litawasilishwa hivi karibuni kwa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo kwa majadiliano kwa kuwa Jumuiya hiyo inachukua nafasi ya uongozi kuhakikisha kuwa yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 hayatatokea tena popote katika eneo hilo.