Kundi la Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji limepeleka timu kwenye eneo ilipotokea ajali mbaya ya kivuko jumapili iliyopita.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, timu hiyo itafanya kazi ya kutathmini na kuunga mkono juhudi za kukabiliana na janga hilo zinazofanywa na mamlaka za Msumbiji.
Ajali hiyo ilitokea jumapili karibu na Kisiwa cha Msumbiji katika mkoa wa Nampulaulioko kaskazini mwa Msumbiji.
Afisa utawala wa huko, Silverio Nauaito amesema, kivuko kilichobeba watu 130 waliokuwa waliokimbia Mossuril kwa hofu kufuatia taarifa ambazo hazikuwa za kweli za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Jumatatu jioni, rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema zaidi ya watu 100 wamefariki katika ajali hiyo.