Madaktari wa China watoa huduma ya bure ya matibabu kwa jamii nchini Sudan Kusini
2024-04-12 10:02:05| CRI

Madaktari wa China wametoa huduma za matibabu bila malipo kwa wakazi wa eneo la Nakuten Korok, lililopo Rajaf Payam, kaskazini mwa mkoa wa Juba nchini Sudan Kusini.

Wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ya tumbo, magua na kutoka vipele mwilini tangu mwezi Machi mwaka huu, lakini hawakuweza kupata matibabu sahihi mpaka kikosi cha 11 cha madaktari wa China kutembelea eneo hilo.

Kikosi cha walinzi wa Amani wa China katika Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) kilipendekeza kuanzisha kambi ya matibabu baada ya kuona hali mbaya ya wakazi wa huko.

Katibu wa kijiji cha Nakituen Korok Kusini, Gabriel Ladu, amewapongeza askari wa kulinda Amani wa China na timu ya madaktari kwa kutoa huduma inayohitajika ya matibabu kwa wakazi wa jamii hiyo.