Baraza la Usalama la UM halijafikia makubaliano kuhusu uanachama rasmi wa Palestina
2024-04-12 23:24:22| cri

Mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Bi. Vanessa Frasier ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Malta katika Umoja huo, amesema baraza hilo halijafikia makubaliano kuhusu ombi la Palestina kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa katika mkutano uliofanyika jana Aprili 11. Hata hivyo, Bi. Frasier ameongeza kuwa asilimia kubwa ya wajumbe wameweka bayana msimamo wa kuendelea kuiunga mkono Palestina kupewa uanachama rasmi wa UM.