China yatoa wito wa kuimarisha ushirikiano kwenye biashara ya bidhaa za TEHAMA
2024-04-12 14:30:19| cri

China imewasilisha mapendekezo ya kudumisha utekelezaji mzuri wa “Makubaliano ya teknolojia ya habari” na kuongeza mambo yanayohusika kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO), ambako imetoa wito wa kuimarisha ushirikiano kwenye mambo ya biashara ya bidhaa za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

China imesema katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya TEHAMA duniani inaendelea kwa kasi, pande zote zinataka nchi wanachama wa WTO ziimarishe ushirikiano, kuhimiza kazi husika za WTO ziendane na wakati, kuonyesha zaidi hali mpya kabisa ya sasa ya maendeleo ya sekta hiyo, na kuhimiza zaidi biashara ya bidhaa husika. Kwa hiyo China inapendekeza kuwa WTO itoe ripoti ya biashara ya dunia ya bidhaa za TEHAMA kila mwaka, kujitahidi kuondoa vizuizi vya biashara kwa bidhaa husika, na kuimarisha zaidi mawasiliano kati ya sekta hiyo na watu wanaoweka sera.

Wanachama husika wamesifu mashauri ya China, na kupenda kufanya majadiliano na China kuhusu mambo husika.