Ethiopia yapata zaidi ya dola za Marekani milioni 600 kutokana na mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo katika muda wa miezi minane
2024-04-12 09:30:42| cri

Serikali ya Ethiopia jana imesema imepata dola za kimarekani milioni 617 kutokana na mauzo ya bidhaa maalum za kilimo katika muda wa miezi minane.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Wizara ya Biashara na Ushirikiano wa Kikanda ya Ethiopia, imesema mapato hayo yametokana na mauzo ya nje ya bidhaa zinazofuatiliwa na wizara hiyo kama vile soya, maharage mekundu, na ufuta.

Takwimu kutoka wizara hiyo zinaonyesha kuwa, mapato yaliyoripotiwa ya mauzo ya nje yameongezeka kwa takriban dola za Kimarekani milioni 80 ikilinganishwa na kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha uliopita wa 2022/23.

Wizara hiyo imesema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa kuu za kilimo nchi za nje pamoja na ongezeko la pato la uzalishaji wa mbegu za ufuta nchini humo.