Kenya yazindua mpango wa kukabiliana na ajira ya watoto katika sekta ya kahawa na chai
2024-04-12 09:55:23| CRI

Kenya imezindua mradi utakaokomesha ajira ya watoto katika sekta ya kahawa na chai nchini humo.

Katibu wa kudumu katika Wizara ya Kazi na Ulinzi wa Jamii ya Kenya, Bi Florence Bore amesema, mpango huo unaoitwa “Hatua ya kuharakisha kukomesha ajira ya watoto katika mnyororo wa ugavi barani Afrika”, utatekelezwa katika miaka mitano ijayo kwenye kaunti 4 za vijijini ambako ajira ya watoto ni jambo la kawaida katika sekta ya kilimo.

Bi Bore amewaambia wanahabari huko Nairobi kwamba mradi huo utaongeza juhudi za serikali na nia yake ya kulinda hatma za watoto.

Ameongeza kuwa mradi huo pia utatoa mchango wa kusaidia Kenya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG 8) kuhusu kukomesha ajira ya watoto itakapofika mwaka 2025.