China yaitaka pande husika zijizuie kufuatia Iran kushambulia malengo ya Israel
2024-04-14 12:33:36| CRI

Wizara ya mambo ya nje ya China leo imesema, China inafuatilia Iran kushambulia malengo ya Israel, na kuzitaka pande husika kujizuia ili hali isizidi kuwa mbaya zaidi.

Wizara hiyo inasema, jambo muhimu kwa sasa ni kutekeleza kikamilifu azimio la No. 2728 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na kutatua mgogoro wa Gaza haraka iwezekanavyo. China pia inaitaka jumuiya ya kimataifa hasa nchi zenye ushawishi kufanya kazi ya kiujenzi kwa ajili ya kulinda amani na utulivu wa kanda hiyo.