Maharamia wa Somalia waiachia meli yenye bendera ya Bengladesh na mabaharia wake
2024-04-15 08:30:09| CRI

Meli yenye bendera ya Bengladesh MV Abdullah na mabaharia wake wote ambao walishikiliwa na maharamia wa Somalia kwenye bahari ya Hindi, wameachiwa huru.

Msemaji wa kundi la KSRM linalomiliki meli hiyo, Mizanul Isalm amewaambia wanahabari kuwa wafanyakazi wote 23 pamoja na meli hiyo waliachiwa mapema Jumapili, mwezi mmoja baada ya kutekwa nyara. Wafanyakazi wote wako salama na katika hali nzuri kiafya, na wamewasiliana na jamaa zao.