China yatoa mwito kuepusha hali ya mvutano ya Mashariki ya Kati kuzidi kupamba moto
2024-04-15 09:01:11| CRI

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura kuhusu shambulizi la Iran dhidi ya Israel. Mjumbe wa muda wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amezitaka pande husika kujizuia ili kuepusha hali ya wasiwasi kuzidi kupamba moto.

Balozi Dai ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mapigano kuzidisha hali ya wasiwasi ya kikanda na kuleta athari mbaya kwa nje.

Aprili 1 jengo la ubalozi wa Iran nchini Syria lilikumbwa na shambulizi la anga likisababisha vifo vya watu kadhaa wa upande wa Iran na uharibifu mkubwa wa jengo, tukio ambalo limekiuka vibaya katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, na mamlaka za Syria na Iran.

Balozi Dai amesema, China inafuatilia kupamba moto kwa tukio lililotokea Aprili 13, na inazitaka pande husika kujizuia na kutatua mvutano kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, ili kuepusha hali ya wasiwasi kuzidi kupamba moto.