Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) Imetoa wito kwa pande hasimu nchini Sudan kukomesha vita iliyodumu kwa mwaka mmoja.
Katibu mtendaji wa IGAD Workneh Gebeyehu amezisihi pande zote zinazopambana nchini Sudan kusitisha mara moja uhasama na kutoa kipaumbele katika kutafuta suluhu ya kisiasa kupitia mazungumzo.
Taarifa iliyotolewa na IGAD kwa vyombo vya habari inasema, katibu mtendaji wa IGAD amesisitiza haja ya kuongeza maradufu juhudi za kutatua hali mbaya ya kibinadamu na kukomesha mateso kwa watu, na kutambua athari za mgogoro kwa utulivu wa Sudan na eneo la mpaka.