Rais wa China akutana na chansela wa Ujerumani
2024-04-16 13:56:54| cri

Rais Xi Jinping wa China leo mjini Beijing amekutana na chansela wa Ujerumani Bw. Olaf Scholz.

Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 10 tangu China na Ujerumani zianzishe uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote. China na Ujerumani ni nchi ya pili na ya tatu duniani kwa ukubwa wa uchumi, na kuimarisha na kuendeleza uhusiano wao kuna umuhimu kwa mabara ya Asia na Ulaya, na hata dunia nzima. Hivyo nchi hizo mbili zinapaswa kushughulikia na kuendeleza uhusiano wao kwa mtazamo wa muda mrefu na wa kimkakati, ili kuchangia zaidi utulivu na uhakika kwa dunia.

Scholz amesema, Ujerumani inapenda kuendelea kuimarisha uhusiano na China, kuongeza mazungumzo na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, na kuhimiza mawasiliano ya elimu na utamaduni, mambo ambayo ni muhimu sana kwa Ujerumani, China na dunia nzima.

Viongozi hao pia wamebadilishana mawazo kwa kina kuhusu migogoro kati ya Russia na Ukraine, na kati ya Palestina na Israel.