China yazitaka pande husika ziache kuchukua hatua zinazochochea hali ya wasiwasi nchini Yemen
2024-04-16 11:04:48| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang jana kwenye mkutano wa baraza la usalama kuhusu suala la Yemen, alisema China inafuatilia hali ya wasiwasi kwenye Bahari ya Sham na kuzitaka pande husika zijizuie na kusimamisha hatua zinazochochea hali hiyo.

Balozi Geng amesema hivi sasa, hali ya Yemen bado inakumbwa na changamoto nyingi, na pande husika zinapaswa kushiriki kutatua mgogoro kwa njia ya kisiasa, kuondoa usumbufu na kuhimiza mchakato wa kisiasa unaoongozwa na kudhibitiwa na watu wa Yemen.

Pia amesema China inaunga mkono juhudi za mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Yemen na kuzitaka pande zote haswa nchi zenye ushawishi kwa hali ya Yemen zifanye kazi ya kiujenzi.