China yazitaka pande zote za Libya ziendelee kuhimiza mchakato wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo
2024-04-17 10:40:25| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa balozi Dai Bing amesema China inazitaka pande zote wa Libya zizingatie kulinda maslahi ya taifa, na kuendelea kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo na kuhimiza maendeleo ya mchakato wa kisiasa.

Balozi Dai Bing amesema kwenye mkutano wa baraza la usalama kuhusu suala la Libya, kuwa hivi karibuni pande zote za Libya ziliendelea kufanya mazungumzo kuhusu mchakato wa uchaguzi na kufikia makubaliano mengi. China inaunga mkono juhudi za mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Bw. Abdoulaye Bathily, na kuutaka ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya utekeleze majukumu yake.

China pia imeitaka jumuiya ya kimataifa ifuatilie maombi ya Libya na kuheshimu ukamilifu wa mamlaka na ardhi ya Libya.