Walinda amani wa UM wafanikiwa kuwaokoa watu watano waliotekwa nyara nchini DRC
2024-04-17 09:09:35| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema walinda amani wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) wamefanikiwa kuwaokoa raia watano waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wenye silaha katika jimbo la Ituri, mashariki mwa nchi hiyo. Kabla ya raia hao kusafirishwa na kurudishwa nyumbani kwao, MONUSCO iliwapatia makazi ya muda na huduma ya afya.

Bw. Dujarric ameongeza kuwa walinda amani pia wamepelekwa kwenye eneo moja la uchimbaji madini mashariki-kaskazini mwa mji wa Bunia, ili kuwalinda raia wa eneo hilo kufuatia mashambulizi yanayofanywa na kundi la CODECO, na kusababisha vifo vya raia wanne.