Makadirio mapya ya Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, yanaonesha kuwa mapigano yaliyodumu kwa mwaka mmoja kati ya jeshi la serikali ya Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) yamesababisha asilimia 90 ya watoto milioni 19 wanaofikia umri wa shule nchini humo kushindwa kwenda shule.
Shirika hilo limetoa taarifa ikisema Sudan sasa inakabiliwa na msukosuko mkubwa zaidi wa elimu duniani, na ukatikaji wa elimu unaoendelea utasababisha msukosuko zaidi kwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tawkimu rasmi zilizotolewa na wizara ya elimu ya juu ya Sudan, vita hiyo imesababisha vyuo zaidi ya 100 vya umma na binafsi kufungwa, na kuharibu idadi kubwa ya vyuo vikuu na taasisi za ngazi ya juu.