Waziri Mkuu wa China afanya mazungumzo na chansela wa Ujerumani, na kutoa mwito wa kuhimiza mahusiano ya nchi mbili
2024-04-17 08:45:34| CRI

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amefanya mazungumzo na chansela wa Shirikisho la Ujerumani Olaf Scholz hapa Beijing, na kutoa wito wa kuwepo kwa kiwango kipya cha mahusiano kati ya nchi hizo mbili, kupanua maelewano na kupata matokeo ya kunufaishana kupitia mazungumzo na ushirikiano.

Akikumbusha kuwa huu ni mwaka wa kumi tangu China na Ujerumani zianzishe ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, Bw. Li pia amesema China iko tayari kufanya kazi na Ujerumani kuongeza maelewano kwa njia ya mazungumzo na kupata matokeo ya kunufaishana.

Bw. Scholz amesema Ujerumani inaishukuru China kwa kutekeleza sera ya kuingia bila visa kwa raia wa Ujerumani nchini China, na pia iko tayari kuweka urahisi kwa raia wa China kutembelea Ujerumani. Pia amesema Ujerumani inapinga vitendo vya kujilinda kibiashara na iko tayari kushirikiana na China kuweka uwanja sawa wa ushirikiano na kupanua ushirikiano wa pande mbili.