IGAD yazindua zana mpya ya kuboresha ufuatiliaji wa ukame
2024-04-18 08:42:06| CRI

Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD), imezindua chombo kipya cha kuboresha ufuatiliaji na kukabiliana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Kifaa hicho cha kiuvumbuzi kinachojulikana kama "Ufuatiliaji Ulioimarishwa kwa Ukame wa Afrika Mashariki," kinatarajiwa kuleta mapinduzi katika utabiri wa ukame katika kanda hiyo, na kuwezesha uingiliaji kati kwa wakati ili kuepusha majanga ya kibinadamu.

Mtaalamu wa mfumo wa data na taarifa za kijiografia katika Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na Maombi (ICPAC) kinachosimamiwa na IGAD Bw. Jason Kinyua, amesema zana mpya ya ufuatiliaji wa ukame itawawezesha watunga sera na jumuiya za mitaa katika kanda kujiandaa vyema kwa athari mbaya kama vile shinikizo la ukosefu wa maji na uhaba wa chakula.