Jukwaa la nne la Uwekezaji la Cameroon lafunguliwa Douala
2024-04-18 08:47:56| CRI

Jukwaa la nne la Uwekezaji la Cameroon, likiwa ni mkutano muhimu unaofanyika kila baada ya miaka miwili ukiwaleta pamoja maofisa waandamizi wa serikali, washirika wa maendeleo, na wadau wa biashara kutoka sehemu mbalimbali duniani, lilifunguliwa jana Jumatano mjini Douala.

Jukwaa hilo lililoandaliwa na Wakala wa Kukuza Uwekezaji wa Cameroon (CIPA), linalenga kuimarisha uwezo wa kuzalisha bidhaa mbadala za zile zilizoagizwa kutoka nje, kupitia kuhamasisha na kuelekeza uwekezaji kwenye sekta muhimu zikiwemo mpunga, mahindi, samaki, maziwa na mafuta ya mawese.

Kaimu maneja mkuu wa CIPA Donatus Boma amesema lengo kuu ni kuhamasisha wewekezaji wa ndani na kuvutia uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja kwenye kuhimiza uzalishaji na uchakataji wa bidhaa nchini.