Jiji la Dar es Salaam laorodheshwa katika nafasi ya 16 kwa utajiri barani Afrika
2024-04-18 10:33:11| cri

Kwa mujibu wa ripoti ya kampuni ya utafiti ya New World Wealth na kampuni ya Henley & Partners’, Mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania umeorodheshwa katika nafasi ya 16 kwa idadi ya mamilionea wa dola.

Ripoti ya Utajiri wa Afrika 2024 inaonesha kuwa Dar es Salaam ina watu 1,200 wenye utajiri wa thamani ya zaidi ya dola milioni moja (Sh2.5 bilioni). Ripoti hiyo ya Utajiri wa Afrika ya 2024 zaidi inajumuisha watu wenye cheo cha ukurugenzi, Mkurugenzi Mtendaji, mwanzilishi na mshirika.

Miji miwili ya Afrika Kusini Johannesburg (12,300) na Cape Town (7,400) inaongoza kwa idadi ya mamilionea wa dola barani Afrika ikifuatiwa na Cairo yenye 7200, kisha Nairobi yenye 4,400 na Lagos inakamilisha 5 Bora ikiwa na mamilionea 4,200.

Ingawa Tanzania imeshuka kwa namba 10 kwa mara ya kwanza ikiwa na mamilionea wapatao 2,300, ina watu wanne ambao wana utajiri wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 100 nyuma ya nchi zenye nafasi ya juu za Afrika Kusini yenye 102, ikifuatiwa na Misri yenye 54, Nigeria yenye 23, Kenya 16 huku Morocco ikimaliza tano bora kwa kuwa na 32.