Mkutano wa kutangaza maonesho ya 7 ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa za China (CIIE) na Jukwaa la Kiuchumi la Hongqiao, ulioandaliwa kwa pamoja na Idara ya Maonesho ya CIIE, ubalozi wa China nchini Zimbabwe, na Shirika la Kukuza Biashara la Zimbabwe, ulifanyika jana mjini Harare, Zimbabwe. Maofisa wa serikali ya Zimbabwe na wawakilishi wa wafanyabiashara walihudhuria mkutano huo.
Naibu mkurugenzi wa Idara ya Maonesho ya CIIE ya China Bw. Song Shangzhe alisema, awamu sita zilizopita za maonesho ya CIIE yalikusanya bidhaa za ubora wa juu kutoka Zimbabwe na Afrika, na kutoa mchango katika maendeleo makubwa ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Zimbabwe na China na Afrika kwa ujumla, na kwamba CIIE iko tayari kuyasaidia makampuni ya Zimbabwe kuingia kwenye soko la China.