Tanzania yapoteza dola za kimarekani milioni 5.9 kutokana na uvuvi haramu kutoka mwaka 2019 hadi 2023
2024-04-19 09:21:25| CRI

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Tanzania imepoteza takriban Shilingi bilioni 15.2 (sawa na dola za kimarekani milioni 5.9) kutokana na uvuvi haramu kutoka mwaka 2019 hadi mwaka 2023.

Ripoti hiyo inayohusisha kipindi cha mwaka 2022/2023 imesema asilimia kubwa ya uvuvi haramu umefanywa kwa kutumia mashua zisizosajiliwa au zisizo na leseni katika Bahari ya Hindi, pamoja na maziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa, ikidokeza kwamba asilimia 72.99 ya mashua za uvuvi nchini Tanzania hazijasajiliwa au hazijapata leseni.