Rais wa Kenya athibitisha kifo cha mkuu wa jeshi katika ajali ya ndege
2024-04-19 08:54:02| CRI

Rais William Ruto wa Kenya amethibitisha kuwa mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla alikuwa miongoni mwa makamanda wakuu 10 waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea jana katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Kenya.

Rais Ruto amesema Bw. Ogolla alikuwa ndani ya helikopta ya KDF na wanajeshi wengine 11. Helikopta hiyo ilipaa kutoka kwa shule ya msingi ya eneo hilo katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet ilipoanguka na kuwaka moto muda wa saa 8:20 alasiri. Rais Ruto alisema Ogolla aliondoka Nairobi asubuhi ili kuwatembelea wanajeshi waliotumwa katika eneo hilo lenye matatizo kupambana na majambazi.