Mradi wa maji na usafi unaofadhiliwa na China wazinduliwa nchini Kenya
2024-04-19 08:53:27| CRI

Mradi wa maji unaofadhiliwa na Jumuiya ya Watu wa Jiangsu ya Urafiki na nchi za Kigeni na Mfuko wa Amity, shirika huru la kijamii la China, umezinduliwa jana huko Nairobi, Kenya.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Chama cha Kikomunisti cha China cha Kamati ya Mkoa wa Jiangsu na makamu mkuu wa mkoa wa Jiangsu Bw. Ma Xin, amesema mpango wa maji unalenga kupanua upatikanaji wa maji safi kwa wakazi katika makazi yasiyo rasmi ya Kenya. Ameongeza kuwa mpango huo ni hatua muhimu kwa Jiangsu kusaidia nchi za ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ kuboresha maisha na ustawi wa watu kupitia nguvu za kijamii.

Mbunge wa Nairobi Bibi Esther Passaris amesema mradi huo utachangia kuboresha upatikanaji na usimamizi endelevu wa maji na usafi kwa watu wa Kenya. Amesema hadi sasa ushirikiano kati ya Kenya na China umeleta manufaa, ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa maji safi ya bomba katika makazi yasiyo rasmi.