Tamasha la 14 la Kimataifa la Filamu la Beijing lafunguliwa
2024-04-19 14:15:37| cri

Tamasha la 14 la Kimataifa la Filamu la Beijing (BJIFF) lilianza Alhamisi katika mjini Beijing, likiwakaribisha watengenezaji filamu kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili maendeleo ya filamu na kukuza mawasiliano ya kitamaduni katika tasnia hiyo.

Wajumbe wa jopo la 14 la Tuzo za Tiantan za BJIFF za mwaka huu, wakiongozwa na mwongozaji filamu wa Serbia Emir Kusturica kama rais wa jopo hilo, walihudhuria kwenye hafla ya ufunguzi.

Jumla ya filamu 1,509 kutoka nchi na maeneo 118 zilituma maombi ya kushirikishwa kwenye shindano hilo mwaka huu, na 15 zimeteuliwa kuwania Tuzo ya Tiantan.

Katika kipindi cha tamasha hilo la siku tisa, zaidi ya filamu 250 za ndani na kimataifa zitaoneshwa katika kumbi 27 za sinema mjini Beijing, na katika Mji jirani wa Tianjin na Mkoa wa Hebei.

Tamasha hilo lililozinduliwa mwaka 2011, linalenga kuongeza mawasiliano kati ya wadau wa sekta hiyo duniani, na limekuwa likifuatiliwa zaidi duniani kutokana na soko linaloshamiri la filamu la China.