Watu 391 wafariki kwa kipindupindu na homa ya dengue nchini Sudan
2024-04-19 14:24:37| cri

Wizara ya afya ya Sudan jana imesema, jumla ya watu 391 wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu na homa ya dengue katika mwaka mmoja wa vita nchini humo.

Waziri wa Afya wa Sudan Bw. Haitham Mohamed Ibrahim amesema, licha ya vita hiyo, wizara ya afya imetoa miongozo ya dharura kwenye majimbo yaliyokumbwa na ugonjwa wa kipindupindu, ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Akizungumzia juhudi za Wizara hiyo katika kutoa huduma za msingi za afya, Waziri huyo amesema kipaumbele cha kwanza cha Wizara yake ni kutoa huduma za afya kwa majimbo yote na sehemu zote.