UNECA: Afrika iko nyuma kufikia malengo ya SDGs wakati umaskini na changamoto za madeni vikiongezeka
2024-04-19 10:42:41| CRI

Katibu mtendaji wa Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA Bw. Claver Gatete, amesema Afrika bado iko nyuma katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs, ingawa imeonesha ustahimilivu mkubwa dhidi ya athari zisizotokana nayo.

UNECA imetoa taarifa ikimnukuu Bw. Gatete akisema, katika miaka mitano iliyopita umaskini na njaa vimekuwa vinaongezeka barani Afrika, wakati changamoto za madeni, kifedha na tabianchi zikiendelea kuongezeka.

Bw. Gatete amesema tangu mwaka 2010 wameshuhudia kuongezeka kwa kiwango cha madeni kwa asilimia 180. Kwa bara zima la Afrika deni la umma kwa sasa limefikia asilimia 66 ya pato la taifa, na gharama kubwa za kulipa madeni zinabana matumizi ya lazima katika sekta za afya, elimu na hatua za tabianchi.