Marekani yapiga kura ya turufu dhidi ya ombi la Palestina kuwa mwanachama rasmi wa UM
2024-04-19 08:38:00| CRI

Marekani imepiga kura ya turufu dhidi ya ombi la Palestina kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwenye Baraza la Usalama.

Baraza hilo lenye wajumbe 15 walipigia kura rasimu ya azimio linalotoa pendekezo kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa “nchi ya Palestina itambuliwe kama mwanachama rasmi wa Umoja huo”.

Rasimu ya azimio hilo ilipata kura 12 za ndio, wajumbe wawili hawakupiga kura, na kura moja ya turufu kutoka Marekani.

Jana Alhamisi, mjumbe maalumu wa Rais wa Palestina, Ziad Abu Amr, alipohutubia Baraza la Usalama alisema kuridhiwa kwa azimio hilo kutawapa wapalestina matumaini ya “kuwa na maisha yenye heshima ndani ya nchi huru”.