Timu ya 25 ya matibabu ya China nchini Sierra Leone, pamoja na wataalamu wa matibabu kutoka Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi cha China, wamezisaidia jamii za wenyeji nchini humo kupambana na ugonjwa wa malaria.
Madaktari wa China walianza programu ya wiki mbili Jumatano wiki hii kutoa huduma za matibabu za bila malipo kwenye Jamii ya Rogbangba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Malaria Duniani, inayoangukia Aprili 25.
Kiongozi wa timu ya matibabu ya China, Lu Chaoqun amesema malaria ni tishio kubwa kwa maisha ya watu nchini Sierra Leone, na programu yao inalenga kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kuhimiza usafi kwenye jamii.