Filamu ya China iliyooneshwa nchini Kenya kuchochea uhusiano kati ya China na Kenya
2024-04-22 09:02:33| CRI

Kufuatia kukua kwa uhusiano kati ya China na Kenya, filamu ya China ilioneshwa Jumapili huko Nairobi, nchini Kenya, na kujizolea sifa nyingi sana kutoka kwa watazamaji.

Filamu hiyo, inayoitwa “Mameya wa China: Kutoa Demokrasia,” ilikuwa ni moja ya filamu zilizooneshwa wakati wa Tamasha la tisa la Kimataifa la Filamu za Nje ya Afrika ambalo hutumika kama jukwaa la kukuza mawasiliano ya kiutamaduni kupitia filamu za sinema.

Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nje ya Afrika, Mumbi Hinga, alisema kuwa tamasha la mwaka huu ambalo linaendelea kwa siku nne, limevutia filamu 40 kutoka nchi 35 duniani. Hinga alisema kuwa filamu ya China ilichaguliwa na jopo lake la majaji kwa sababu imeangazia mada muhimu ya namna viongozi wa serikali wanavyoendelea kuwajibika kwa wananchi kwa kuhakikisha wanatoa huduma za umma kwa ufanisi.

Elvis Kigen, ambaye alitazama filamu hiyo ya dakika 106, alisema kuwa filamu hiyo ilisaidia kuondoa dhana kwamba demokrasia ya magharibi ni aina ya utawala bora ikilinganishwa na mifumo mingine kote duniani.