Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri na ofisa wa UM waonya mashambulizi ya Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi
2024-04-22 09:00:27| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry na mwandaaji maalumu wa ripoti wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya haki za binadamu katika maeneo yaliyokaliwa ya Palestina, Francesca Albanese Jumapili walijadili njia za kupunguza mateso ya watu wa Palestina kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israel.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imemnukuu Shoukry akisema kuwa wanasisitiza umuhimu wa kusimamisha mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Gaza, kuendelea kutoa msaada wa pande zote kwa watu wenye uhitaji wa eneo hilo, na kukomesha vurugu na mashambulizi yanayofanywa na walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Albanese alieleza wasiwasi wake mkubwa juu ya hali mbaya ya haki za binadamu ya watu wa Palestina kutokana na vitendo vya Israel katika ardhi ya Palestina inayokaliwa.