Umoja wa Afrika watoa salamu za rambirambi kutokana na ajali mbaya ya boti nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
2024-04-22 09:03:11| CRI

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat ametoa rambirambi zake kwa familia zilizoathiriwa na ajali kubwa ya boti nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) iliyotokea Ijumaa jioni.

Faki aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, uliojulikana kama Twitter kwamba mshikamano wao wote uko kwa serikali na watu wa CAR kufuatia kuzama kwa boti kwenye mto Mpoko na kusababisha vifo na majeruhi.

Habari zimesema kuwa idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo imeongezeka hadi 62.