Mtoto mmoja afariki kutokana na maporomoko ya udongo magharibi mwa Burundi
2024-04-22 23:42:06| cri

Mtoto mmoja amefariki kutokana na maporomoko ya udongo yaliyotokea ijumaa jioni na kuharibu nyumba 497, pamoja na bwawa la umeme lililoko kanda ya Gitaza, wilaya ya Muhuta, mkoa wa Rumonge kusini magharibi mwa Burundi.

Katibu wa gavana wa mkoa huo Abdul Ntiranyibagira amesema, kijiji cha Gabaniro ndicho kimeathirika zaidi na maporomo hayo, ambapo mtoto mmoja wa miaka minne alifariki na nyumba 497 kuharibika, na kuwaacha watu 2,485 bila makazi.

Amesema zaidi ya ekari 500 za mashamba pia zimeharibiwa katika maporomoko hayo katika kijiji cha Gabaniro na vijiji vya jirani.