Waziri Mkuu wa Uingereza asema wahamiaji nchini humo wataanza kupelekwa Rwanda ndani ya miezi mitatu
2024-04-23 10:07:01| cri

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amesema, makubaliano ya kuhamisha wahamiaji kati ya nchi hiyo na Rwanda yataanza kutekelezwa ndani ya kipindi cha wiki 10 hadi 12 ambapo ndege ya kwanza inayobeba wahamiaji hayo itaondoka Uingereza kuelekea Rwanda.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa mwezi Desemba mwaka jana mjini Kigali, Rwanda, na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili, yanalenga kufufua Uhusiano wa Uhamiaji na Maendeleo ya Uchumi (MEDP), ambao ulipingwa na Mahakama Kuu ya Uingereza mwezi Novemba mwaka jana.

Utaratibu huo unalenga kuwahamisha watu walioingia Uingereza kwa kutumia boti ndogo na kuwapeleka Rwanda ambako wataweza kuomba hifadhi.