PowerChina yazindua ujenzi wa kituo cha nishati cha photovoltaic nchini Algeria
2024-04-23 23:06:15| cri

Shirika la Ujenzi wa Nishati la China (PowerChina) limeanza ujenzi wa kituo cha umeme wa photovoltaic kaskazini mwa Nigeria, ambacho kina uwezo wa kuzalisha megawati 220 za umeme.

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ujenzi huo unaofanyika Bir Naam, mkoa wa Biskra, kusini mashariki mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers, ilihudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini wa Algeria, Mohamed Arkab.

Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 16, na mradi huo utatoa ajira zaidi ya 600 wakati wa ujenzi wake, na kuongeza nguvu ya umeme katika gridi ya taifa hilo.