Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) Aretas Lyimo amesema kuwa Tanzania imekamata dawa za kulevya kilo 767.2 zikiwemo heroini kilo 233.2, methamphetamine kilo 525.67 na skanka kilo 8 katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga katika wiki mbili za kwanza za mwezi Aprili.
Amesema, mamlaka hiyo pia iliwakamata washukiwa 21 wanaohusishwa na dawa hizo, ambapo dawa hizo nyingi ziliingizwa nchini humo kupitia Bahari ya Hindi.