Rais wa Nigeria atoa wito wa kupambana na ugaidi wa kikanda ili kutatua masuala ya umaskini na kutokuwa na usawa
2024-04-23 09:28:46| CRI

Rais Bola Tinubu wa Nigeria Jumatatu alitoa wito wa kuanzisha kituo cha kikanda cha kupambana na ugaidi, ambacho kitakuwa kituo cha kupeana taarifa za kijasusi, kuratibu opresheni na kujenga uwezo barani Afrika.

Akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi barani Afrika uliofanyika Abuja nchini Nigeria Tinubu amesema, Afrika lazima ichukue hatua za kina katika kupambana na ugaidi, na kuondoa mizizi inayosababisha tatizo hilo, ikiwa ni pamoja na umaskini, kutokuwa na usawa na kutokuwa na haki kwenye jamii.

Aliongeza kuwa mambo muhimu katika kupambana na ugaidi kwa pamoja ni kuanzisha kituo cha kikanda cha kupambana na ugaidi kitakachofanya kazi kikamilifu, na kuunda kikosi cha kikanda kitakachokuwa tayari kwa shughuli hiyo.