Rais Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi mjini Chongqing
2024-04-23 15:23:42| cri

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi mjini Chongqing kuanzia tarehe 22 hadi 23 mwezi huu. Kwenye ziara hiyo, Rais Xi ametembelea Kituo cha Ugavi cha Kimataifa cha Chongqing, eneo la makazi la mtaa wa Xiejiawan wilayani Jiulongpo, na Kituo cha Uendeshaji na Usimamizi wa Mji wa Kidijitali cha Chongqing. Lengo la ziara hiyo ni kufahamu hali ya mji huo katika kuharakisha ujenzi wa ushoroba mpya wa kuunganisha bahari na nchi kavu katika sehemu ya magharibi, kufanya maboresho kwa mji na maisha ya wakazi, na kuinua kiwango cha usimamizi wa mji.