Tamasha la kutangaza utalii na utamaduni wa mkoa wa Shanxi nchini China lafanyika nchini Morocco
2024-04-24 10:34:30| cri

Tamasha la utalii na utamaduni wa mkoa wa Shanxi nchini China limefanyika jumatatu katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, jumatatu wiki hii, kwa lengo kuutambulisha mkoa wa Shanxi kwa jamii ya Morocco.

Gavana wa Shanxi, Jin Xiangjun amesema, tamasha hilo ni fursa ya kuboresha mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Morocco katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii na utamaduni.

Katibu mkuu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni na Mawasiliano nchini Morocco, Mustapha Messoudi ameeleza matumaini yake kuwa, tamasha hilo litafungua fursa ya kuwezesha mawasiliano kati nchi za Kiarabu na China.

Naye Balozi wa China nchini Morocco, Li Changlin amesisitiza kuwa, uhusiano wa China na Morocco uko katika wakati mzuri katika historia, ukiwakilisha fursa nyingi za ushirikiano wa pande mbili.