Viongozi wa Afrika watoa wito wa kuongezwa kwa thamani ya madini ya bara hilo
2024-04-24 09:34:59| CRI

Nchi wanachama wa Shirika la Mkakati wa Madini Afrika (AMSG) Jumanne walifanya Kongamano la Uwekezaji wa Madini huko Lilongwe, nchini Malawi, ambapo walizitaka nchi za Afrika kuongeza thamani ya madini kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi.

Katibu Mkuu wa AMSG Moses Engadu alitoa wito huo wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la siku mbili, uliofanywa na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, ambapo aliangazia changamoto kuu kwa Afrika zikiwemo usafirishaji wa madini yakiwa ghafi badala ya kusafirisha madini yaliyochakatwa ili kupata faida kubwa.

AMSG ni mpango wa nchi 16 za Afrika unaolenga kuwezesha ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo endelevu ya madini muhimu.