Mazungumzo mapya ya Marekani kuhusu “Kupita kiasi kwa uwezo wa uzalishaji wa China” yatafanikiwa?
2024-04-24 10:46:38| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara yake ya pili nchini China kuanzia tarehe 24 April. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi za nje, Bw. Blinken atafuata hatua za Waziri wa Fedha Janet Yellen, na kuendelea kuzungumzia kile kinachoitwa “ Kupita kiasi kwa uwezo wa uzalishaji” wa China.

Bibi Yellen alipozungumzia suala hili wakati alipotembelea China alisema, uwezo wa uzalishaji wa China umezidi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya soko la ndani la China, na pia umezidi yale ya soko la kimataifa, hali ambayo itaweza kusababisha uuzaji nje wa bidhaa kwa bei chini, na kuleta athari mbaya kwa makampuni na wafanyakazi nchini Marekani na nchi nyingine.

Lakini baadhi ya wachambuzi wa uchumi nchini Marekani hawakubaliani na kauli hii ya Bibi Yellen, kwani inakwenda kinyume na kauli za msingi za uchumi ambazo nchi za Magharibi zimetetea kwa zaidi ya miaka 200.

Imeonekana kuwa viwanda ambavyo China ina sifa kubwa zaidi ikilinganishwa na Marekani, vinatajwa na Marekani kuwa “viwanda vyenye uwezo mkubwa wa kupita kiasi wa uzalishaji”. Madhumuni ya hatua hiyo ya ujanja ya Marekani ni kushusha hadhi ya viwanda vyenye sifa kubwa zaidi vya China kwa madai kuwa ni “tishio”, ili kuzuia maendeleo ya viwanda hivyo.

Lakini ukweli ni kuwa, uzalishaji wa viwanda vya magari ya nishati mpya haupiti kiasi, bali bado kuna safari ndefu ya kukua, na ili kufikia lengo la kuondoa hewa chafu duniani, bado inahitajika uwezo mkubwa zaidi wa magari ya nishati mpya.